Tundu Lissu atinga Polisi kufuata gari lake


Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amefika kwenye ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, RPC Martin Otieno akitaka kuliangalia gari lake ambalo anasema alishambuliwa akiwa nalo.


Lissu amefika leo Alhamisi, Februari 9, 2023, huku akisema kuwa alikuwa amewasiliana na RPC kwa ajili ya kwenda kuliona gari lake hilo ambalo hata hiivyo bado hajafanikiwa kuliona akielekezwa kurudi wakati mwingine kutokana.

Hata hivyo, Lissu kwenye maelezo yake amebainisha kuwa ameelezwa kuwa RPC Otieno ameenda kwenye tukio la ajali ya basi kugongana na lori huko Kongwa mkoani Dodoma.

Lissu ameeleza kuwa ameambiwa arejee baadaye ili aweze kuonana na RPC Otieno ili aweze kupata utaratibu wa kuliona gari lake, pamoja na kujua namna ambavyo anaweza kukabidhiwa.

Chanzo: mwanachidigital


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo