Katika taarifa tofauti, mwanamke kutoka nchini Uganda alinaswa akiwa na mtoto aliyeibwa na ambaye alitoweka mnamo Februari 8, 2023.
Mtoto huyo wa miezi miwili aliibiwa kutoka Kyegegwa na aliokolewa siku chache zilizopita kwa usaidizi wa CCTV.
Taarifa ya Polisi nchini Uganda ilionyesha mshukiwa Sharifa Linda, ni raia wa Congo aliyemteka nyara mtoto huyo na kumpeleka kwa mpenzi wake.
Polisi walisema Linda alimdanganya mpenzi wake kwamba alikuwa mjamzito na siku ambayo alinaswa, alikuwa akimpeleka mtoto huyo.