Mkuu wa Wilaya ya Mjini Magharibi Unguja, Rashid Simai Msaraka amepiga marufuku Wafanyabiashara wa Wilaya hiyo kuweka midoli yenye nguo zisizo za staha nje ya maduka yao.
DC Msaraka ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na Mfanyabiashara maeneo ya Kwahani Zanzibar akiwa ameweka midoli hiyo nje ya duka ikiwa imevalishwa nguo ambazo zinadaiwa kupotosha maadili ya Zanzibar hususani kwa Watoto pindi wanapoona midoli hiyo imevishwa nguo hizo.
DC Msaraka ameiambia AyoTV kuwa maarufuku hiyo imetokana na Watoto na Vijana kuona vitu visivyo na staha na kupelekea kuvuraga akili za Vijana wa Zanzibar "Hatuwakatazi kuwa na midoli hiyo wala hatuwakatazi kufanya biashara hizo ila biashara hizo zifanywe ndani na zisiwekwe nje, Mtu anayetaka kuvaa nguo hizo avae mwenyewe anajua utaratibu gani wa kuzivaa na wapi azivae"
Chanzo:Ayo TV