Babu wa miaka 80 adaiwa kumnajisi mjukuu wake wa miaka 8

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia Luhende Tugwa (80), mkazi wa Kijji cha Ihapa Kata ya Old Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga kwa tuhuma za kumnajisi mjukuu wake mwenye miaka minane.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Janeth Magomi amesema tukio hilo limetokea jana Jumatano, Februari 8, 2023 majira ya saa 4.30 asubuhi baada ya mtoto huyo kutoka shule.

Kamanda Magomi amesema kuwa, siku ya tukio mke wa mzee huyo alikuwa shamba na ndipo mzee huyo alipotumia nafasi hiyo kutekeleza unyama huo.

Kamanda Janeth amesema kuwa wanamshikilia mzee huyo kwa hatua zaidi za kisheria ili kujibu tuhuma zinazomkabili,huku akiitaka jamii kuendelea kukemea vitendo vya ukatili na kuwafichuwa watu wanaoendelea kufanya ukatili kwa wanawake na watoto.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo