Hakimu awataka wazazi kuwakagua watoto sehemu za siri

Kutokana na kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto, wazazi wameshauri kuwa na tabia ya kuwakagua watoto wao wanapotoka shule.


Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora, Jovit Katto amesema hali ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto kwa sasa ni mbaya na hatua za kudhibiti hali hiyo lazima zichukuliwe.

Akizungumza wakati wa kutoa elimu kwa umma katika wiki ya sheria, hakimu Katto amesema wazazi wanapaswa kuwakagua watoto wao wanapotoka shule na hasa kwa wale wanaotumia usafiri wa bodaboda na bajaji waendapo au kurudi shuleni.

Ameeleza kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la matukio ya watoto kufanyiwa vitendo vya ukatili ikiwemo kulawitiwa jambo ambalo linaendelea kukua siku hadi siku huku watoto wakiathiriwa na matukio hayo.

"Kumekuwa na ongezeko kubwa la kesi za ulawiti dhidi ya watoto jambo ambalo linapaswa kushughulikiwa ili kulimaliza," amesema.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo