Mkulima na Mkazi wa Kijiji cha Kising'a Mkoani Iringa aliyejulikana kwa jina la Frank Kigomba (31) amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na fidia ya Tsh.Laki 5 kwa kosa la kumnajisi Mdogo wake wa kuzaliwa tumbo moja mwenye umri wa miaka 15 baada ya kushauriwa na Mganga wa kienyeji kuwa akifanya hivyo atapata utajiri.
Akiongea na Wanahabari wa Iringa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Allan Bukumbi amesema Mtuhumiwa alikamatwa na kufikishwa Mahakamani January 05,2023 baada ya kufanya kosa hiloJanuary 02,2023 saa 10 alfajiri ambapo alikwenda chumbani kwa Mdogo wake na kumuita kwa nia ya kwenda kuingiza mbao ndani ya kijumba kibovu nyumbani hapo na kisha kumvua nguo na yeye alivua suruali na akamuingilia.
Kamanda Bukumbi amesema uchunguzi umeonesha Mtuhumiwa alishauriwa na Mganga wa kienyeji kuwa akifanya mapenzi na Mdogo wake atapata utajiri ambapo akiwa Mahakamani amekiri kutenda kosa hilo na kuhukumiwa kifungo.
Bukumbi ametoa wito kwa Wananchi kushirikiana na Polisi na kuendelea kutoa taarifa za uhalifu ili ziweze kushughulikiwa kwa haraka.