Waziri Mbarawa aagiza tozo zipungue

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof Makame Mbarawa amesema kuwa zifanyike jitihada za haraka ili kupunguza vumbi la makaa ya mawe lililopo katika Bandari ya Mtwara na maeneo jirani ya bandari hizo kwa kuboresha mazingira ya kutunzia makaa hayo.

Kauli hiyo ameitoa leo Ijumaa Desemba 2, 2022 katika ziara ya siku moja aliyofanyika mkoani hapa ambapo amesema wafanye haraka ili kutatua changamoto hizo kwa kutengenenza miundombinu itakayosaidia kupunguza vumbi hilo.

"Ili kutibu vumbi hilo tumeamua kujenga kituo cha kuhifadhia makaa ya mawe yatakaa sehemu moja na kuweka ukanda maalum wa kusafirisha makaa ya mawe mpaka kwenye melini Ili kupunguza vumbi la makaa ya mawe.

"Msitumie ule utaratibu wa kawaida wa manunuzi ambao unachukua miezi sita tumieni vifungu vya sheria ya manunuzi zitumieni Ili ufanyike utaratibu wa haraka wa kujenga ukanda huo naamini TPA wanazo fedha," amesema Mbarawa.

“Bandari ya Mtwara inatakiwa kuiendelezwe ili iwe kituo kikubwa cha usafirishaji kwenye ukanda huu siyo mikoa hii hata kwa nchi jirani ili kuhakikisha kuwa mizigo yote iwe inapitia hapa kwnaza inatakiwa iwe na vifaa vya kisasa kitakachosaidia kupakia mizigo na kupakua mizigo imefungwa hapa,” amesema.

“Kwa mara kwanza katika historia ya nchi yetu tumeleta mashine kubwa ambazo tumefunga Mtwara na Dar es Salaam na tumeleta vifaa vingi vya kisasa tunauwezo wa kubeba meli yenye mzigo wa tani 60,000 hili ni jambo kubwa kwa bandari yetu,” amesema Prof Mbarawa.

“Pia tunacho kituo cha kupokelea mafuta mengi hapa na kupeleka hata nchi za jirani yapo mafuta yanaenda malawi ni vema yakapitia hapa zamani yalikuwa yanakuja kidogo kutokana na miundombinu sasa yanakuja mengi” amesema.

“Iko haja ya kupunguza baadhi ya tozo zinazosimamiwa na TPA mfano zanzibar wanalipa mil 60 lakini sasa ni mil 30 gharama ya kupakia na kupakua mzigo asalimia 70 imepungua ili kuhakikisha kuwa Bandari ya Mtwara inakuwa kivutio” amesema Mbarawa.

Naye Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Juma Kijavala amesema kuwa Mamlaka hiyo ina mkakati ya kujenga bandari mpya ya Mgao.

“Tutaharakisha utaratibu sasa tunaenda kuangalia namna bora ya kufanya ili mkandarasi apate lakini tunaenda kujenga Bandari ya Kisiwa Mgao kwaajiili ya kusafirishia mizigo kama saruji, Makaa ya mawe na sulfa kuweka facility,” amesema Mhandisi Kijavala.

Chanzo: Mwananchi 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo