Serikali inakopa kwa ajili ya maendeleo na si vinginevyo


Mjumbe wa Halmashauri Kuu Mkoa wa Lindi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Peter Msaki, ametoa maoni yake kuhusu ishu ya mikopo.


Msaki amesema:

“Kuhusu hoja ya deni la taifa nafikiri kama Watanzania tuanze kuwaza tofauti juu ya dhana ya mkopo kwanza tukubaliane mkopo ni maendeleo siyo kwa sababu nyinginezo kama kusema hata nchi tajiri zinakopa bali ni ukweli ili ufanye maendeleo kwa wakati na ukubwa wake lazima uwe na fedha nyingi za pamoja.

"Sasa makusanyo yetu kwa mwaka hayatoshi kufanya matumizi ya kawaida na maendeleo kwa wakati mmoja hivyo kukopa ni lazima, hili hatuwezi kukwepa hata kama chama kingine kitachukua serikali watakopa tu, na mimi nasema kama kuna uwezekano wa kukopa fedha zaidi tukope zote zikatekeleze miradi yote ya maendeleo inayogusa maisha ya Watanzania.

"Mkopo ni hela yako unachukua kabla na kulipa kwa riba baada ya makusanyo yako.

"Badala ya kujadili ukubwa wa deni la taifa, tujadili tija ya deni hilo. Je, thamani ya deni na maendeleo yetu vinalingana? Je, fedha inayokopwa inatumika vizuri kama ilivyokusudiwa?

"Nafikiri hapa ndipo mjadala unapaswa kuwa na si vinginevyo.

"Leo kuna hoja ya bei ya mabehewa kutokuendana na ubora wa mabehewa yenyewe. Kama ni kweli hawa ndiyo wakushughulika nao ndiyo wanafanya thamani ya deni la taifa isionekane kwenye maendeleo ya watu.

"Baada ya kujadili tija ya deni la taifa, tujadili kuhusu matumizi yetu. Lazima tuwe na matumizi yenye tija kulingana na uwezo wetu, pili nidhamu ya kusimamia fedha za umma mwisho mkakati wa kupunguza deni la taifa hasa baada ya kufikia maendeleo.

Kwa kuwa makusanyo yetu ni madogo; na mahitaji yetu ni makubwa na mengi; tufanye haya:

1. Tukubaliane ni yapi tuyakopee siyo kila wizara inaibuka na kukopa. Tuwe na vipaumbele.

2. Tupanue uwazi wetu katika kukopa na uwazi wetu katika kutumia fedha hiyo ili watu wapige kelele wakiona ubadhirifu."


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo