Mifugo 2035 yakamatwa Hifadhi ya Taifa Tarangire



Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi, TARANGIRE-MANYARA 


Jeshi la Polisi Kupitia kikosi cha kuzuia na kupambana na wizi wa mifugo na migogoro ya wakulima na wafugaji Nchini kwa kushirikiana na  hifadhi ya Taifa Tarangire limefanikiwa kukamata Ng’ombe 2035 walioingia hifadhini kwa ajili ya kulisha mifugo hiyo ambapo ni kinyume na Sheria.


Akitoa taarifa hiyo leo december 22 kamanda wa Polisi Kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo nchini kamishina msaidizi wa Polisi ACP SIMON PASUA amesema Jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa sita kwa kosa la kuingiza na kulisha mifugo hiyo ndani ya hifadhi.


Watuhumiwa waliokamatwa ni Muliyo Lekashu (25),Moringe Mpeleke (30),Sabaya Sumuni (38), Lemburis Roika (45),Terengo Kondeki (70),Saruni Rosio (43) wote ni wakazi wa Emboreti wilaya ya Simanjiro.


Kamanda Pasua amebainisha kuwa Jeshi hilo linaendelea na upelelezi na mara baada upelelezi kukamilika watuhumiwa watafikishwa katika vyombo vya sheria.


ACP PASUA ametoa wito kwa wafugaji kufuata sheria za matumizi bora ya ardhi vingine amesema kuwa Jeshi la Polisi halito fumbia macho vitendo vya uhalibifu wa rasmali za taifa.


Kwa uoande mhifadhi mwandamizi katika hifadhi ya taifa Tarangire SC WILLIAM MAREGES amesema wao kama wadau wakubwa wauhifadhi hawato sita kuwachukulia hatua wale wote watakao husika na uharibifu wa rasilmali za taifa


Ameongeza kuwa wataendelea kuzilinda na kuhifadhi rasilmali za taifa kwa masilahi makubwa ya taifa


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo