SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limesema litaanza kutoza ushuru magari yanayoingia au kupita kwenye hifadhi za taifa kuanzia mwezi Machi mwakani.
Hayo yalibainishwa na Ofisi ya Kamishna wa Uhifadhi wa Tanapa kupitia taarifa kwa umma jana. Kwa mujibu wa Tanapa, kanuni za Shirika Na.255 za mwaka 1970 zilizofanyiwa marejeo mwaka 2018, zinalitaka shirika hilo kutoza magari yote yanayoingia au kupita hifadhini kwa kuzingatia uzito wa gari bila mzigo.
Tanapa iliwataka wadau wote wakiwemo wakala wa utalii, wasafirishaji wenye magari yanayoingia au kupita kwenye hifadhi za taifa na wananchi kuhakikisha wanapata cheti kinachothibitisha uzito wa magari kutoka Mamlaka ya Vipimo nchini (WMA).
-
Ilieleza kuwa cheti hicho cha kila gari kitahitajika kuthibitisha uzito wa gari kila linapoingia au kupita hifadhini kuanzia Machi Mosi mwakani. “Ni matumaini yangu kuwa wadau wote mtatumia muda huu hadi ifikapo Machi 1, 2023 kupata cheti husika kwa kila gari ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji,” ilisema taarifa hiyo.
Endelea kuchangia nauli ya Elia kupitia namba ya M-pesa (0757551799), ama NMB (53010000837), jina SYLIVESTER DOMASA LUGUTU.