Maajabu: Marehemu afufuka huko Kigoma, alizikwa Aprili 2022

Kijana Henry James (28) Mkazi wa Kijiji cha Kandaga Wilayani ya Uvinza Mkoani Kigoma ambaye aliyefariki na kuzikwa mwezi Aprili 2022, amepatikana akiwa hai December 28, 2022 na kuungana tena na Familia yake huku akisema “mlipokuwa mnazika nilikuwa nimesimama pembeni kwenye mti”


Mama mzazi wa Kijana huyo ameiambia @AyoTV_ kuwa Mwanae alifariki kwa kugongwa na gari tarehe April 19 na kuzikwa tarehe 20.

"Huyu ni Mtoto wangu kabisa na aliyefariki alikuwa ni huyu ila nashangaa kurudi kwake wakati sisi tulimzika hii naona ni miujiza ya Mungu, kwasababu tulipokuwa tunamzika nililia sana nikimwambia Mungu naomba unisaidie sababu nilipata misiba ya kufatana ya Watoto wangu wawili hadi nikahisi vibaya"-Scholah Bukuru, Mama Mzazi.

Henry James alionekana Kijiji jirani cha Kaseke ambapo alionwa na Jirani aliyekuwa akiishi nae kipindi cha nyuma ndipo akaamua kuwapigia Ndugu zake simu na Mwenyekiti wa Kijiji ambapo nyumba anamoishi Kijana huyo imegeuka kama sehemu ya utalii kutokana na Watu kutoka Vijiji jirani kumiminika kwenda kumtazama.

Kamanda wa Polisi Kigoma Philemon Makungu amethibitisha kuwa na taarifa za tukio hili na kusema Polisi wataanza kufanya uchunguzi ikiwemo kuruhusu uchunguzi wa kisayansi pamoja na kufukua kaburi.

TAZAMA VIDEO HII HAPA
Chanzo: Ayotv


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo