Bwana harusi ampiga mkewe wakati wakifunga ndoa kanisani

Wakiwa wamesimama kwenye madhabahuni kwa ajili ya harusi yao ya kanisani, bwana harusi ghafla alimpiga bibi harusi wake kofi usoni.


Tukio hilo lisiloelezeka lilinaswa katika video iliyoshirikiwa na @esthernice2 kwenye TikTok.

Kabla ya kofi hilo, bwana harusi alionekana kumsogelea mke wake kana kwamba anataka kumpiga busu. Lakini hatimaye hakumbusu na akakubali kumpiga kofi.

Haijabainika ni nini huenda kilichochea hatua yake kwani sauti ya video hiyo haikueleweka na klipu hiyo haikuzidi sekunde 17. Kioja hicho kilizua hisia mseto miongoni mwa watu.

Haya ni maoni ya baadhi ya watu mitandoani kufuatia video hiyo;

TarlishaB alisema: "Huyu mwanamke yuko taabani..... anatabasamu tu kwa uchungu.... iwapo huyu jamaa anaweza kumtandika katika madhabahu ina maana atafanya hivyo popote.. sisi wanawake tuwe makini."

Oluwadamilola alisema: "Hii ni nini?"

Jae Daniels alisema: "Samahani. Nilipepesa macho na kukosa kuona kitu hapa. Nasubiri sehemu ya 2 wakati eneo la maankuli litageuka sarakasi na kisha mazishi."

watezydseer alisema: "Jamani, kwani huyu bibi harusi hana kaka? Kwa sababu ningekuwa kakake hilo kanisa halingekalika hata kidogo. Bwana harusi angenitambua."

Wakati huo huo, Legit.ng hapo awali iliripoti kwamba bibi harusi alimpiga bwana harusi wakati wa sherehe yao. Katika video hiyo fupi iliyodumu kwa sekunde 19 tu, bibi harusi ndiye aliyekuwa wa kwanza kumshushia kichapo mchumba na kila aliyekuwepo alishangazwa na kitendo chake hicho.

Kuhusu nini kilisababisha kofi hilo la moto, inaonekana bwana harusi alikuwa akimlisha bibi harusi kwa nguvu na alijaribu kumzuia. Alimpiga mwanamume huyo na jamaa akamrejeshea jambo lililozua vita vikali baina ya wawili hao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo