Bodaboda Wamwogesha Mwenzao Baada ya Wateja Kulalamika kuwa ni Mchafu

Waendesha bodaboda wa Nakuru wamemwogesha mwenzao na kumnunulia nguo mpya za ndani baada ya wateja kulalamikia uvundo mkali wa mwili wake.


Waendeshaji hao wa bodaboda kutoka Molo waliwapoteza wateja kwa siku nyingi ambao walilalamikia usafi wao na hivyo kuamua kuchunguza kati yao ni nani ambaye hakuwa akioga.


Wakizungumza na Inooro TV, waendeshaji hao walisema walikwenda mtoni kumwogesha baada ya kubaini kuwa ni muda mrefu tangu aoge. Walichanga pesa kati yao ili kumnunulia mwenzao sabuni na vitu vingine.


"Wateja walikuwa wamelalamika kwa muda mrefu kwamba sisi ni wachafu. Walipoacha kuja kwetu, ilibidi tujue ni nani kati yetu ambaye hakuwa akioga," mmoja wa waendeshaji bodaboda alisema. “Tunashangaa kwa sababu tukiwa mtoni tukimwogesha tuligundua hana hata nguo za ndani na tumemnunulia mpya,” mhudumu mwingine wa bodaboda alibainisha. 


Baada ya mwili wake wote kupakwa sabuni, na kuchanwa na wenzake, bodaboda huyo alitoka nje ya mto akiwa amezaliwa upya. “Nko freshi barida,” alisema. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo