Mjane kutoka magharibi mwa Kenya amelia kwa uchungu kukosa mlo wa ugali kwa wiki kadhaa kwa sababu ya umaskini uliokithiri na kwamba hana mtu wa kumtunza
Licha ya kuwa mama wa watoto watano, Lorna Indekhwa anaishi maisha ya upweke ambapo hutegemea waamaria mema kumsaidia katika mambo ya msingi.
"Sijala ugali kwa wiki nne, nimekuwa nikinywa tu maji ya moto kusitiri njaa," alisema. Haya yote yalijitokeza kwenye Idhaa ya YouTube ya Jim Nduruchi wakati kikundi cha wasamaria walipotembelea eneo la Indekhwa kusaidia katika kutokomeza funza katika makazi ya watu.
Walikuwa wakienda kwenye boma lingine walipokutana na bibi kizee dhaifu ambaye aliwaambia kuhusu shida yake. "Ninaonekana kama mtu asiye na mtoto; kifo kilimchukua mwanangu ambaye alikuwa ametoka tu kuhitimu na alikuwa akirudi nyumbani. Alikufa katika ajali ya barabarani," alisema. Indekhwa alizaa watoto 15 na hadi sasa, amewazika watoto 10 kati yao. Wawili wamehama na ni mmoja tu anayeishi katika boma pamoja naye.
“Hata maji sina,” alisema kikongwe huyo. Kwa majuma yote mawili amekuwa akitumia maji ambayo aliletewa na watu wa kanisa ambapo kando na hilo walimfulia nguo zake. Mnamo Juni, Wakenya walianza kulalamikia gharama ya juu ya bidhaa za kimsingi, ikiwa ni pamoja na mafuta ya kupikia, unga wa mahindi, unga wa ngano na sukari. Hali hiyo iliweka shinikizo kwa bidhaa za matumizi ya nyumbani.
Kuongezeka kwa bei ya mafuta kumewafanya Wakenya kutumia pesa nyingi zaidi katika usafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine anbapo matatu walitangaza kupandisha nauli kote nchini.
Wanamtandao walidai matatizo yalitokana na kukithiri kwa rushwa na usimamizi mbovu wa serikali unaofanywa na viongozi walioahidi kuboresha maisha yao.