Wanafunzi wa shule ya msingi Tulieni iliyo katika kijiji cha Tulieni kata ya Ndono wilaya ya Uyui mkoani Tabora wamekuwa wakilazimika kutumia karatasi ngumu na miti kujisafisha chooni kutokana na kukosekana kwa maji hivyo kuiomba serikali kuharakisha maboresho ya miundombinu shuleni hapo.
Wanafunzi wa madarasa wawili tofauti wanalazimika kusoma kwenye chumba kimoja kutokana na idadi ya madarasa kutokukidhi mahitaji.
Hali ya vyumba vya madarasa haikidhi mahitaji,madawati nayo hayatoshelezi na tayari wananchi walianza ujenzi wa vyumba vingine vya madarasa miaka miwili iliyopita wakitegemea serikali iunge mkono ili wanafunzi wasome kwenye mazingira mazuri huku pia kukiwa na suala la uhaba wa maji, wakiomba hatua zifanyike ili kulinda afya za wanafunzi hao.
Chanzo:eatv.tv