Zaidi ya wanafunzi 130 wanatumia darasa moja katika shule ya msingi Luhama kata ya Bangwe Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza kutokana na upungufu wa madarasa katika shule hiyo.
Shule hiyo ambayo ina wanafunzi 1, 306 ina vyumba vyumba vya madarasa 10 huku mahitaji yakiwa vyumba 39 ikiwa na upungufu wa madarasa 39.
Hali hiyo inawasababishia adha wanafunzi wakati wa masomo yao inayotokana na mlundikano mkubwa katika darasa moja.
Hayo yamebainishwa leo Jumamosi Novemba 12, 2022 na mwalimu mkuu wa shule hiyo, Peme Nteba wakati wa mahafali ya 39 ya shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1976.
Nteba amesema kuwa kwa sasa wana upungufu wa madarasa 29 hali inayosababisha wanafunzi zaidi ya 130 kutumia darasa moja tofauti na matakwa ya darasa moja kwa wanafunzi 45, hivyo amewaomba wadau wa elimu kujitokeza kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye shule hiyo ili kuwanusuru wanafunzi kurundikana.
"Shule ina upungufu wa vyumba vya madarasa hivyo nawaomba wazazi wa wanafunzi, waliosoma shule hii miaka iliyopita, wananchi na wadau wa elimu katika maeneo haya kuona umuhimu wa kujitolea ili kuhakikisha ujenzi wa madarasa unakamilika” amesema Nteba.
Via Mwananchi
