Wakurugenzi punguzeni safari - RC Mtaka

Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ameagiza wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo kupunguza safari zao za mara kwa mara zisizokuwa za lazima na badala yake watulie kwenye vituo vyao vya kazi ili waendelee kutafiti zaidi njia za kuwasaidia wananchi pamoja na kujenga vyanzo vipya vya mapato kukuza uchumi wa halmashauri zao.


Mtaka ametoa maagizo hayo wakati wa kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe mkoani humo.

"Haya mambo ya wakurugenzi kusafiri safiri punguzeni,vitu vingi tunafanya vya kawaida wakati kamkoa ketu ni kadogo mno kwa hiyo ni lazima mtulie kwenye vituo mpate muda, sasa unakuta tunaenda kufunga mwaka darasa la saba anashangilia,form four anashangilia na wewe decision maker unashangilia yaani hamna utofauti,hio hapana lazima mje na kitu cha tofauti"amesema Anthony Mtaka


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo