Majaliwa Joseph, kijana aliyewezeshwa kuokolewa kwa watu 26 katika ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea katika Ziwa Victoria November 6 mwaka huu amefika bungeni jijini Dodoma akiwa ni miongoni mwa wageni walioalikwa Leo Novembea 11, 2022.
Baada ya kutambulishwa Bungeni na Spika wa Bunge, Dr. Tulia Ackson alimpongeza mama wa kijana Majaliwa Jackson kwa kazi nzuri ya kumlea na kumpa ujasiri wa kujiamini pamoja na mazingira aliyonayo jambo ambalo lilimuibua mbunge wa jimbo la Mkalama, Francis Mtinga kuomba muongozo wa spika kuhusu baba mzazi wa kijana huyo pia apongezwa jambo ambalo lilizua shangwe miongoni mwa wabunge
Spika Tulia alitoa muongozo wake kwa kumwambia Mbunge huyo yeye ndiyo ampongeze Baba Mzazi wa Majaliwa jambo ambalo mbunge huyo alilifanya
“Mimi nimempongeza mama yake kwa sababu maalumu, na habari ya baba nimempa nafasi Mbunge wa Mkalama amempongeza, tusichanganye mambo Bunge limempongeza mama”-Spika Dr. Tulia Ackson
