Moto wasababisha hasara Tanesco, Wenyewe watoa Kauli

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) wilaya ya Makete mkoani Njombe limeelezea kusikitishwa na vitendo vya moto unaoanzishwa na baadhi ya watu ambao umekuwa ukiunguza miundombinu yake na kusababisha hasara kwa shirika hilo


Akizungumzia suala hilo kwenye kikao cha baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo, Meneja wa TANESCO wilaya ya Makete Henricko Renatus amesema kumekuwa na uharibufu unaosababishwa na watu kuchoma moto na kuunguza nyaya na nguzo hali inayopelekea umeme kukatika na wao kubeba lawama

Amesema hali hiyo inasababisha fedha zinazotolewa kwa ajili ya maboresho mbalimbali ya umeme, kuacha kufanya kazi iliyokusudiwa na matokeo yake fedha hizo zinapelekwa kutengeneza miundombinu iliyoharibiwa na moto na kusababisha mambo mengine kukwama, hivyo kuwaomba madiwani kuwasaidia kuwaelimisha wananchi

 

Gwerino Mwasanga ni Diwani wa kata ya Ikuwo na Christopher Fungo ni diwani wa kata ya Iniho wamezungumzia suala hilo la moto lilivyoleta athari ikiwemo kuunguza miundombinu ya Tanesco na hata uharibifu wa mazingira, huku pia wakitoa ushauri kwa shirika hilo wanapofanya usafi wa njia ya umeme kwa kukata miti, yale masalia wayaweke mbali na miundombinu hiyo ili moto ukija na kukuta hakuna matawi ya miti madhara huwenda yakapungua


Hivi karibuni kumeripotiwa matukio ya moto kuunguza miundombinu ya umeme katika maeneo mbalimbali lakini pia na kuunguza misitu ya watu jambo linalochangia athari kubwa na kwa upande wa Wilaya hatua mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa ikiwemo uzinduzi wa kamati za kupambana na matukio ya moto zilizozinduliwa hivi karibuni na mkuu wa Wilaya ya Makete.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo