Mama na mtoto wakamatwa wakituhumiwa kuiba Njombe

Mama na mtoto wake wakazi wa Mji wa Kambarage mkoani Njombe wamenusurika kupata kichapo kutoka kwa wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi, na kujikuta wakipokea adhabu ndogondogo wakati wakipelekwa kwenye ofisi za mtaa huo


Kilichowafanya wakutane na dhahama hiyo ni kutokana na kutuhumiwa kuiba vitu mbalimbali kwenye maduka na nyumba za watu katika mtaa huo

Tazama Video hapa

Kwa mujibu wa Mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Dorisi Mchami, na Blandina Kayombo wameeleza kuwa mtoto wa mama huyo amekuwa akiiba vitu mbalimbali zikiwemo laptop, flash na vifaa vya simu pamoja na nguo zilizoanikwa majumbani na kumpelekea mama yake ambaye amekuwa akitafuta wateja na kuuza ili kupata fedha za kujikimu huku vitu vingine wakivitumia nyumbani kwake


Wamesema mara baada ya kumkamata mtoto huyo aliweza kuwapeleka nyumbani kwao anakohifadhi lakini hawakuvikuta mpaka walipotoa adhabu kwa mama yake na kuamua kuonesha alikokuwa amevifukia shambani nje ya nyumba yake kutokana na kuhofia kukamatwa

France Sanga ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Kambarage amesema katika mtaa wake suala la ulinzi ni la mtu mmoja mmoja kwa kuwa askari walionao hawatoshi na kudai katika mtaa wake wezi na wadokozi wapo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo