Madiwani Makete wacharukia barabara kutengenezwa vipande vipande

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mkoani Njombe wameelezea wasiwasi wao kuhusu matengenezo ya barabara kuchelewa kuanza kutokana msimu wa mvua umewadia, hivyo kupata wasiwasi na kazi hiyo kufanyika kwa kiwango

 

Katika Kikao cha Baraza la madiwani leo Novemba 1, 2022 madiwani hao pia wameelezea masikitiko yao ya barabara kutengenezwa kwa vipande vifupi vifupi na kusema hali hiyo ni kama haileti tija

 

Osmund Idawa na Raymond Mgaya ni Baadhi ya madiwani waliotoa maoni yao kuhusu hoja ya barabara na kusema ni afadhali barabara chache zikatengenezwa kilomita nyingi kuliko kutengeneza barabara nyingi kwa vipande vidogo vidogo


Mhandisi John Kawogo kutoka ofisi ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wilaya ya Makete ametolea ufafanuzi huo kwa kusema fedha zinazotolewa ni kwa ajili ya matengenezo na fedha hizo zinakuja kidogo tofauti na walivyopanga kwenye bajeti hivyo wanalazimika kutumia fedha hizo kwa uchache hivyo hivyo

 

Kuhusu Barabara ya Lupila Kipengere ametolea ufafanuzi kuwa baada ya mkandarasi kumaliza kutengeneza barabara ya Ibaga alikwenda Luwumbu na kwa sasa amebakiwa na mradi huo wa barabara ya Lupila Kipengere hivyo atakwenda kuitengeneza barabara hiyo


Hawa Ahmad ni Mwenyekiti wa Kikao hicho ametoa Meneja wa TARURA Kuyafanyia kazi mapendekezo na ushauri uliotolewa na baraza hilo huku akimtaka kutoa vipaumbele kwa barabara ambazo hazipitiki kwa kuwa sio mgeni na barabara za wilaya ya Makete


Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Makete William Makufwe ameishauri TARURA kutoa zabuni kwa wakandarasi wengi badala ya mkandarasi mmoja kupewa barabara nyingi hali inayochangia matengenezo ya barabara hizo kuchelewa kuanza.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo