Bwana Harusi Ambeba Bi Harusi, Msaidizi Wake kwenye Bodaboda Siku ya Harusi

Maoni yamemiminika kwenye video ya jamaa ambaye ni mhudumu wa bodaboda aliyembeba mkewe kwenye pikipiki siku yao ya harusi.


Katika video ya TikTok iliyopakiwa na @Mujunimedardmujuni, mwanamume huyo kwa fahari alipanda pikipiki akiwa na mkewe na kipusa mwingine ambaye ni msaidizi wake.



Inaonekana bibi na bwana harusi walikuwa wakielekea kwenye ukumbi wa harusi. Bibi huyo alivaa hijabu, huku mwanaume huyo akiwa amevalia suti na tai. Hata hivyo, bado haijafahamika iwapo mwanamume huyo ni mhudumu wa bodaboda au ikiwa yeye na mkewe waliamua tu kutumia pikipiki siku yao ya harusi.


Kwingineko, karibu na nyumbani, msafara wa harusi ulikuwa umeunda msongamano mdogo wa magari huku wanandoa hao wakielekea nyumbani kwa mrembo kulipa mahari.


Magari ya mamilioni ya fedha ya bwana harusi ya fahari yaliyojumuisha Toyota Lexus iliyofanana kama ile ya Rais William Ruto yalikuwa kwenye msafara huo. Wanamtandao walionyesha kushangazwa, huku wengi wakisema bwana harusi aliweka viwango vya msafara wa harusi. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo