Bashiru aombewa msamaha, "Ninamuombea radhi Dkt Bashiru aliteleza"

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, Lilian Wasira, amemuombea radhi kwa Watanzania na kwa Rais Samia Dkt Bashiru Ally, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM, kufuatia kauli yake aliyoitoa hivi karibuni ya kwamba Rais Samia haupigi mwingi


Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza kwenye kipindi cha Mamamia cha East Africa Radio na kuwaomba Watanzania wamsamehe akiamini kwamba Dkt. Bashiru aliteleza.

"Tunasema mkubwa hakosei anateleza tu, Mhe (Dkt. Bashiru) ameteleza namuombea radhi kwa Mama Samia na Watanzania wamsamehe ila waipuuze ile kauli, ila kama ile kauli alimaanisha na anahisi hakuteleza basi sisi kina mama tutam-dissapoint, sisi akina mama hatutakubali," amesema Mwenyekiti huyo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo