Aliyetangazwa gazetini kuwa kafa, ajitokeza

Kampuni ya Nation Media Group (NMG) inayomiliki gazeti la Daily Nation imeomba msamaha kwa kuchapisha kimakosa tangazo la kifo cha Rosemary Wekosasa.


Tangazo la kifo cha Wekosasa, ambalo kwa sasa limefutiliwa mbali lilikuwa limechapishwa kwa gazeti la Daily Nation' mnamo Novemba 14.


Hata hivyo baada ya tangazo hilo kuchapishwa, Wekosasa mwenye umri wa miaka 67 ambaye alipaswa kuwa marehemu, alitembea hadi ofisi za kampuni ya Nation na kuthibitisha kwamba angali hai. Kampuni hiyo ilifafanua kwamba tangazo hilo lilichapishwa kwa kuzingatia maelezo ya uongo iliyokuwa aimepewa, hivyo basi notisi hiyo ya kifo kusalia kuwa feki.


Kampuni hiyo iliomba radhi kwa Wakosasa na familkia yake ambayo haikuhusishwa kwenye mchakato wa kuchapisha tangazo hilo. "Kampuni hii inatangaza kujuta kuchapisha tangazo hilo na kuomba masamaha kwa Rosemary Wakosasa, pamoja na familia yhake ambayo haikuhusika kivyovyote wakati wa kuchapishwa kwa tangazo hilo. 


"Pia tungependa kuwaomba radhi wanachi kwa jumla kwa hitilafu hiyo, na kwa wale walioshtuka na kupitia aibu ya aina yoyote kufuatia tangazo hilo feki ya kufariki dunia kwa Rosemary," kampuni hiyo ilisema kwenye ombi la msamaha lililochapishwa siku ya Alhamisi, Novemba 17.

Chanzo: TUKO.co.ke 



JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo