Akutwa amefariki dunia kwenye nyumba inayoendelea kujengwa


Mwanaume ambaye hakufahamika mara moja amekutwa amefariki katika nyumba moja inayoendelea na ujenzi wilayani Manyoni mkoani Singida, huku chanzo cha kifo chake kikiwa bado hakijafahamika


Imedaiwa kuwa huenda kifo hicho kimetokea siku kadhaa zilizopita kutokana na mwili huo kukutwa umeharibika.


Akizungumza kwa njia ya simu Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa, amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa bado jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini undani wa kifo hicho.


Kaimu Mganga Mfawidhi hospitali ya wilaya Manyoni Dkt. Ainea Mlewa, amekiri kupokea mwili huo ambao umehifadhiwa katika chumba cha kuhidhia maiti.

Chanzo:EATV


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo