Wakizungumza na mtandao huu kijijini hapo wananchi hao Bw. Efeso Mgaya,
Albart Mbilinyi pamoja na Patriki Malumba ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya
maafa kijijini hapo wamesema Moto huo umeathiri Mali zao ikiwemo ekari kadhaa
za Miti pamoja na eneo la malisho ya Mifugo.
Wamesema kuna wakati walilazimika kulala kwenye maeneo hayo yanayowaka moto ili iwarahisishie kuulima, na pia kuna wakati moto huruka umbali wa kilomita moja na kuanza kuunguza maeneo mengine lakini hadi sasa wamefanikiwa kuuzima japo kuwa hawawezi kujihakikishia kwa asilimia 100 kutokana na visiki vilivyooza ambavyo vingine vimejifukia ardhini kushika moto ambao hulipuka tena endepo kunakuwa na upepo mkali
Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji
cha Makangalawe Bw Batweli Chengula amesema ni kweli wananchi wake wameathirika
pakubwa na moto huo kwani mbali na kuunguliwa na miti yao pia wametumia muda
mwingi kuuzima moto huo badala ya kufanya shughuli za uzalishaji mali tangu
Oktoba 7 mpaka leo Oktoba 12,2022
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Makangalawe Remijus Magere amesema Moto huo umeunguza ekari nyingi za miti ya wananchi ikiwemo waliofadhiliwa na Shirika la Pandamiti kibiashara.
Amesema moto huo ulisababishwa na mama mjamzito mkazi wa kijiji hicho ambaye aliwasha moto bila kibali na baada ya wananchi kufanikiwa kuuzima katika eneo mojawapo,watu wasiojulikana wakachoma moto eneo la machungio ya mifugo kati ya kijiji hicho na kijiji cha Usungilo