Jeshi la Polisi lakanusha madai ya CHADEMA


Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limesema kuwa limesikitishwa juu ya taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuzuia msafara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika katika eneo la Nanenane mkoani Morogoro.

Tazama video hiyo ikionesha mzozo huo hapa chini

Taarifa hiyo iliyokuwa ikisema “Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro wamezuia msafara wa Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika eneo la Nanenane wamezuia kupita barabara ya Morogoro kwa kile walichodai kuwa kuna kikao cha viongozi wa polisi Morena Hotel wakati huo magari mengine yakiendelea kutumia barabara hiyo.”


Jeshi hilo limesema Mnyika hakuzuiwa bali ulikuwa ni utekelezaji wa makubaliano na viongozi wa CHADEMA na hakuna aliyetamka kuwa kuna mkutano wa Jeshi la polisi Hotel ya Morena siku hiyo kama sababu ya kuwazuia wasipite barabara kuu.


Jeshi la Polisi limewaomba Watanzania kupuuzia taarifa hiyo ambayo si sahihi kwa kuwa ni viongozi waliokiuka makubaliano kati yao na Jeshi.





JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo