DIWANI wa Kata ya Kalola wilayani Tabora (Uyui), Sauji Daud na mkewe, Magdalena Richard wamefariki dunia katika ajali ya gari usiku wa kuamkia leo Jumanne Oktoba 25, 2022.
Akizungumza na kituo cha redio CG FM, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Said Ntahondi, amesema, Diwani huyo na mkewe walikuwa katika gari yao binafsi wakitoka Kalola kuja Tabora mjini na ndipo gari lao lilipogongana na gari lingine uso kwa uso na wao kufariki papo hapo.
Amesema miili yao imepelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete kwa ajili ya uchunguzi na taratibu zingine.