Auawa kwa kuchomwa kisu shingo kwenye koromeo na rafiki yake

Kijana Nasoro Almas (22) mkazi wa Mkundi Manispaa ya Morogoro ameuwawa kwa kuchomwa kisu shingo kwenye koromeo na rafiki yake aliyrjulikana kwa jina la Frank chanzo kikiwa ni marehemu kumdai fedha aliyomkopesha Frank kiasi cha 2000.


Mama wa Marehemu Vumila Nassoro amesema tukio hilo lilitokea baada ya mwanae kumdai fedha shilingi 2000 mtuhumiwa na alipomuomba amrejeshee ndipo alikataa na kuibua mzozo uliosababisha mtuhumiwa kuchukua kisu kwenye pikipiki yake na kumchoma shingoni marehemu.

Mwenyekiti wa mtaa wa Mgulu wa ndege Veronika Michael ametbitisha kutokea tukio hilo ambapo amesema tukio hilo limetokea leo majira ya saa kumi na moja alfajiri katika kijiwe na pikipiki kilichopo katika mtaa huo wakati marehemu na mtuhumiwa wakitoka kwenye sherehe ya rafiki yao.

 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo