Vyombo mbalimbali vya habari Nigeria vimeripoti tukio hilo. Mapema Oktoba 31 Davido alionekana kumfundisha mtoto wake huyo kuogelea huku akimpongeza kwa kuimarika kwenye mchezo huo.
Taarifa zinasema Ifeanyi alizama kwenye maji kwa muda mrefu kabla ya wazazi wake kugundua kutokweka kwa mtoto wao. Baada ya kufanyika kwa msako walimkuta Ifeanyia akielea juu ya maji, na kumkimbiza hospitali lakini haikusaidia kuokoa maisha yake.
Davido anakuwa msanii wa pili nchini Nigeria kumpoteza mtoto kwa kuzama kwenye maji hii ni baada ya kutokea kwa tukio kama hilo kwa msanii D'banji mnamo mwaka 2018.
