Mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Majengo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga Amos Justine (7) amefariki dunia huku ndugu zake wawili wakikimbizwa hospitalini baada ya kula matunda yayodhaniwa kuwa na sumu.
Ndugu wa marehemu, Baraka Justine (10) mwanafunzi wa darasa la tatu na Samweli Justine (5) anayesoma darasa la awali katika shule hiyo nao walikula matunda hayo na kuwafanya kuharisha na kutapika hatimaye kulazwa hospitali.
Mwenyekiti wa mtaa wa Majengo wanakoishi watoto hao John Wagi amesema tukio hilo limetokea Oktoba 8, 2022 majira ya saa 10 jioni na maziko ya mtoto huyo yamefanyika Oktoba 9, 2022.