Rais Samia awashangaa vijana wanaohangaika na "Vumbi la Kongo"

 “Tutafika mahali hatujui mume nani, mke nani. Kwa hiyo twendeni tukasimamie hilo…Wavulana mnaonekana mmevaa suti lakini kuna vigenge vya udongo (vumbi) la kongo chungu mzima, Amos (Mkuu wa Mkoa wa Dar) unanitazama huko ndio kunasifika kwa chipsi,” - Rais Samia Suluhu Hassan.

"Kwanini kunakuwa na lishe mbovu? je! nimasuala yaliyoingia ya kimitindo? kwanini watoto wetu wanakuwa hivyo ..wakifika wakati wakuja kuongeza ‘societies’ wanahangaika mara supu ya pweza mara udongo wa kongo (vumbi la kongo). watafiti fanyeni utafiti tatizo hili linaumiza vijana wetu," - Rais Samia Suluhu Hassan.

"Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuboresha mazingira ya kutolea huduma katika sekta ya Afya, sekta ya Elimu, sekta ya Kilimo nanyi ni mashahidi , tumenunua vifaa vingi vya usafiri, vifaa vingi vya kufanyia kazi lengo ni kwenda kumhudumia mwananchi" – Rais Samia Suluhu Hassan.

"Lishe bora ni muhimu kwa jamii hasa kwa makundi ya wajawazito, wanawake, wazee na vijana walio katika rika ya balehe, sasa ukitazama tunaanza na wajawazito kuwapa lishe bora ili watoe watoto wenye afya lakini mtoto naye akishazaliwa tunahitaji kumtunza" – Rais Samia Suluhu Hassan.

"Utafiti wa lishe uliofanyika 2018 unaonesha kuwa kadri nchi ya Tanzania inapambana na matatizo ya lishe pungufu kwa upande mwingine kuna matatizo yanayotokana na lishe inayopitiliza" – Rais Samia Suluhu Hassan.

"Maelekezo yangu kwa Wakuu wa Mikoa na timu zenu mhakikishe fedha inayopangwa kutekeleza afua za lishe zinatolewa kwa wakati" – Rais Samia Suluhu Hassan.

"Niagize pia Waziri wangu wa TAMISEMI wale wote ambao wamezitumia fedha vibaya za lishe ambapo fedha imeingizwa lakini haikuingia kwenye lishe imeingia upande mwingine, hatua zinapaswa zichukuliwe kwa sababu huu ni ukosefu wa nidhamu" – Rais Samia Suluhu Hassan.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo