Polisi: Risasi haichagui sehemu ya kuingia


Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini SACP David Misime, amewataka Watanzania kurudi kwenye misingi ya imani za dini na kuachana na uhalifu hatua ambayo itaepusha matukio ya washukiwa wa uhalifu kupigwa risasi.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 30, 2022, kupitia mjadala uliofanyika kupitia mitandao ya kijamii wakati akijibu swali lililouliza sababu zilizopelekea vijana waliokamatwa kwa tuhuma za panya road kupigwa risasi kwenye makoromeo.

"Kwa ufupi tu kwamba wakati wa mapambano risasi haichagui sehemu ya kuingia, sehemu yoyote inaweza kukupata, cha msingi Nondo atusaidie kwa vijana wenzake awape elimu kurudi kwenye misimamo ya dini zetu kuacha dhambi ambayo sisi polisi tunaiita ni uhalifu, turudi kwenye msimamo wa kuchukia uhalifua kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa," amesema SACP Misime


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo