"Watakufa tu" - Musukuma

Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma amefunguka na kusema kwamba endapo serikali itaendelea kuwafukuza kazi darasa la saba na kuwaajiri 'graduates' kutoka vyuo vikuu ajali hazitaweza kuisha kwani madereva hao wanakuwa na mawazo wanapowaendesha viongozi wenye elimu ndogo kuliko wao.

Musukuma amefunguka hayo akiwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kila Jumatano kupitia ukurasa wa Facebook EATV ambapo amesema kwamba vijana wengi wanakuwa na mawazo makubwa pindi wanapowaendesha viongozi na watumishi kwani anakuwa anawaza muda na gharama mzazi alizozitumia na bado hajapata kazi nzuri ilia isaidie famillia yake.

Akifafanua, Musukuma amesema kuwa 'graduates wengi wamekuwa wakishuhudia wazazi wakihangaika kuwatafutia pesa ili wasome wapate hata degree moja lakini mwisho wa siku wanateseka katika kupata ajira.

Aidha Msukuma ameshangaa namna ambavyo vyeti vya udereva vimekuwa vikitolewa na chuo cha usafirishaji ambapo amehoji kwa nini wanachukua pesa za wanafunzi wa darasa la saba ilhali kwenye ajira watu wenye kiwango cha elimu hiyo wanabaguliwa.

" Unamfukazaje darasa la 7 kazi? Unataka aendeshe wa chuo kikuu. Unampa graduate kazi ya kuendesha gari na mwisho wa siku anakudikia wewe unapokea simu ya madili ya mamilioni mawazo yake yanaenda mbali lazima mfe tu kwasababu anamawazo mengi kulingana na ule muda aliyoupoteza shuleni " amesema.

"Mawaziri na watumishi wengine hata hii ajali iliyotokea juzi wataanguka mno.

Watauawa kwasababu haiwezekani mtu ame-graduate kwa shida halafu unampa kazi ya kuendesha gari. Lazima mfe " Msukuma.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo