Wanaume wawaomba Msamaha wanawake waliowachimbisha Kaburi

Na Rehema Matowo GEITA, Tanzania
WANAUME wa mtaa wa Bwihegule kata ya Mtakuja mjini Geita, wameiomba Serikali na wanawake msamaha kwa kitendo cha kuwalazimisha wanawake wa mtaa huo kuchimba kaburi wakiwatuhumu kuwa wachaw

Wakati wengine wakiomba msamaha, asilimia kubwa ya wanaume wa mtaa huo wanadaiwa kukimbia makazi yao wakihofia kukamatwa baada ya kupata taarifa ya ujio wa kamati ya ulinzi na usalama kujua sababu za wanawake kupewa adhabu ya kuchimba kaburi.
Tukio la kaburi kuchimbwa kwa ajili ya kusitiri mwili wa Mzee Nkangiko Vigume (57) lilitokea April 24 saa saba mchana, baada ya agizo lililotolewa na mtemi wa mtaa huo kufuatia kikao cha dharura cha kujadili matukio ya vifo vya ghafla vya wanaume vinavyotokea kisha kuonekana tena mtaani baada ya kuzikwa.
Vigume alifariki April 23 majira ya saa moja usiku baada ya kuumwa kichwa ghafla, inadaiwa uamuzi wa kuwalazimisha wanawake hao kuchimba kaburi ulitokana na matukio mengine ya wanaume sita kuugua ghafla na kufa.
Maiti ya mzee huyo ilidaiwa kuonyesha vituko kama kuweka mkono kifuani na sehemu za siri, hali iliyowafanya wazee hao kuamini mwenzao hakufa kifo cha kawaida.
Madhara
Wakizungumza katika mkutano ulioandaliwa na mkuu wa wilaya ya Geita, Herman Kapufi, baadhi ya wanaume wakizungumza kwa niaba ya wenzao walisema kitendo walichofanya waliona sahihi lakini sasa wameona madhara yake na kuiomba jamii iwasamehe.
“Mkuu wa wilaya kweli hasira hasara, lile tukio la maiti kuonyesha vituko lilitusikitisha na kutushtua, ndiyo maana tukatoa adhabu ili iwe fundisho hatukujua kama ni makosa lakini sasa tumeelewa tunawaomba mtusamehe na nyie wanawake mambo hayatajirudia tena,” alisema Yusuf Elias.
Naye Kapufi alilaani kitendo kilichofanywa na wanaume hao na kuwataka waachane na imani potofu zinazochochea uvunjifu wa amani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo