Sitarudi nyuma kisa Suguta - John Heche

Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia (CHADEMA), John Heche amefunguka na kusema kufuatia kifo cha mdogo wake Suguta Chacha ambaye aliuwawa kwa kuchomwa kisu na askari polisi basi yeye haturudi nyuma kupigania haki za watu ili haki na usawa katika taifa viweze kushamiri

Heche amesema hayo leo Mei 4,2018  siku moja baada ya kupumzisha mdogo wake kwenye nyumba yake ya milele na kusema kuwa kifo cha mdogo wake huyo ambaye amekufa kinyama kinazidi kumpa nguvu na sababu ya kupigania haki. 
"Pumzika kwa amani Suguta, kifo chako cha kinyama kinanipa sababu zaidi ya kuendelea kupigania. Utawala wa sheria haki na usawa katika taifa letu. Sitarudi nyuma nitapambana mstari wa mbele wakati wote kwa heshima yako na kwa heshima ya Watanzania wote wanaopenda kuona nchi yetu inaongozwa vizuri" 
Aidha Heche aliwashukuru watu mbalimbali ambao waliweza kujitokeza kumpumzisha mdogo wake huyo kwenye nyumba yake ya milele na kusema kuwa wamewapa faraja sana 
"Asanteni Watanzania wote na Wanatarime kwa jinsi ambavyo mmekua faraja kwa familia yetu katika kipindi hiki kigumu endeleeni kupiga kelele kukemea uovu huu unaozalisha chuki katika Taifa letu.Pumzika kwa Amani “Simba”" 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo