Matukio Yote ya Rais Magufuli Hii leo Mkoani Morogoro

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa Daraja kubwa la Magufuli lenye urefu wa mita 384 linalopita katika mto Kilombero mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mkewe Mama Janeth Magufuli, Viongozi mbalimbali wa Dini, Serikali, Wabunge wa mkoa wa Morogoro na Viongozi wengine, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Daraja kubwa la Magufuli lenye urefu wa mita 384 linalopita katika mto Kilombero mkoani Morogoro.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali mara baada ya kufungua Daraja kubwa la Magufuli lenye urefu wa mita 384 linalopita katika mto Kilombero mkoani Morogoro.PICHA NA IKULU




 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mang’ula kona katika Wilaya ya Kilombero wakati akiwa njiani kuelekea kufungua Daraja kubwa linalopita katika mto Kilombero (Daraja la Magufuli lenye urefu wa M384) lililopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kiberege wakati akiwa njiani kuelekea kufungua Daraja kubwa linalopita katika mto Kilombero (Daraja la Magufuli) lililopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mang’ula wakati akiwa njiani kuelekea kufungua Daraja kubwa linalopita katika mto Kilombero (Daraja la Magufuli) lililopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika msiba wa mwanafunzi wa Chuo cha Ardhi, James Gerald mara baada ya kutoa rambirambi wakati akiwa njiani kuelekea kufungua Daraja kubwa linalopita katika mto Kilombero (Daraja la Magufuli) lililopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mang’ula Mrindoko Msangi mara baada ya kumkabidhi kiasi cha Shilingi milioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule hiyo. Mwanafunzi huyo alielezea kwa ufasaha kero inayowakabili shuleni hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kwenye msiba wa mwanafunzi wa Chuo cha Ardhi, James Gerald mara baada ya kutoa rambirambi wakati akiwa njiani kuelekea kufungua Daraja kubwa linalopita katika mto Kilombero (Daraja la Magufuli) lililopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanakijiji wa Sanje( hawapo pichani ) wakati akiwa njiani kuelekea kufungua Daraja kubwa linalopita katika mto Kilombero (Daraja la Magufuli) lililopo katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo