Kikwete aishauri serikali ya Rais Magufuli

Mbunge wa Chalinze kupitia CCM, Mh. Ridhiwani Kikwete amefunguka na kuishauri serikali ya serikali ya Rais Magufuli kuwapa kazi vijana wa kitanzania waliobobea katika masuala ya 'project management' ili waweze kusimamia vizuri miradi ya maji ambayo itakayoweza kuzaa matunda mazuri

Ridhiwani Kikwete ametoa kauli hiyo leo Mei 08, 2018 Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 24 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati alipokuwa akichangia kwenye hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ambayo imeweza kuzua gumzo kubwa kwa Wabunge wengi wakilalamikia miradi mbalimbali kushindwa kutekelezwa mpaka hii leo.
"Kinacholalamikiwa kikubwa zaidi katika suala la maji ndani ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji inayoongozwa na Mhandisi Isack Kamwelwe ni 'poor project management' ambayo ipo ndani ya wizara hiyo. Haiwezekani miradi ya maji kwa mfano nikizungumzia wa Chalinze ambao mpaka sasa una zaidi ya miaka 15 kila siku tumekuwa tukizungumzia mradi huo huo",amesema Ridhiwani Kikwete. 
Pamoja na hayo, Mbunge "Mhe. Waziri Kamwelewe sasa nina imani baada ya kumaliza kupitisha bajeti hii, unaweza ukaenda kuliangalia vizuri hili, nina imani pia kuna vijana wazuri wa kitanzania waliosomea 'project management' ambao tukiwapa kazi za kusimamia'project' hizi wanaweza wakatufanyia kazi iliyokuwa nzuri zaidi. Lakini ule utaratibu wa kuenda kuwapa hela moja kwa moja wakandarasi kama ambavyo umefanya pale Chalinze ndio ambao umetufikisha hapa".
Kwa upande mwingine, Ridhiwani Kikwete amesema ni jambo la kawaida kwake kuishauri serikali katika masuala mbalimbali japo kuwa mengine haifanywi kazi ipasavyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo