Mbunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amemshauri Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Simon Sirro kuwa anapaswa kufanya kazi yake na kuwa makini kwani ipo siku wabunge wa CCM watamgeuka
Lema amesema hayo siku kadhaa baada ya kuibuka kwa mijadala bungeni kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea nchini ikiwa pamoja na masuala ya ulinzi na usalama ambapo baadhi ya wabunge walilinyooshea vidole jeshi la polisi kushindwa kushughulikia baadhi ya mambo ikiwa pamoja na kuchunguza sakata la Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kupigwa risasi, kutekwa na kupotea kwa baadhi ya watu akiwepo mwandishi wa habari Azory Gwanda, Ben Saanane na Simon Kanguye.
"IGP umeona mijadala bungeni, CCM hawana aibu nimekuwa nao bungeni kwa miaka nane, walipomsifu Seth wa IPTL na wengine nilikuwepo na walipokuja geuka nilishuhudia, tumeeleza uhalifu mkubwa dhidi ya ubinadamu, kuna siku uhalifu huu utakuwa hadharani. Play smart brother" alisema Godbless Lema