Ngombe 12 wanaosadikiwa kufa wamekutwa wakichinjwa ndani ya lori
eneo la mtaa wa Wazo kwa ajili ya kusambazwa kwenye mabucha ya
ngo’mbe.
Akizungumza na MCL Digital leo Mei 13, mmoja wa mashuhuda Issa
Ibrahim amesema wakati anaelekea msikitini saa 10 alfajiri aliliona gari
aina ya lori limesimama pembezoni mwa barabara na alipolisogelea
aliwaona watu wakiwachuna ng’ombe waliokufa.
Amesema aliwahoji na kuwakataza wasiendelee kuwachuna ngombe
hao kwa kuwa dini hairuhusu kula vibudu lakini watu hao walikaidi na
kuendelea kazi yao.
“Wale watu walikuwa wengi kila mmoja alikuwa na kisu chake huku
wakichuna ngombe hao, kwa kuhofia usalama wangu nilipiga simu
msikitini ndipo walikuja eneo hili ili tuungane tuweze kuwakamata
lakini wote walikimbia na kuacha nyama zao kwenye gari,” amesema
Ibrahim.
kwa mara na ndiyo maana hivi karibuni mmiliki wa machinjio ya Wazo
alimfukuza kazi mchinjaji mkuu baada ya kupingana na kitendo cha
kuchinja ngombe waliokufa.
“Leo hii tunaona ng’ombe 12 wamekufa kibudu na wanaendelea
kuwachuna kwa ajili ya kupelekwa kwenye mabucha
Chanzo:MCL Digital
Chanzo:MCL Digital
