ACT wapingana na Rais Magufuli

Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kuwaruhusu wanafunzi wa vyuo vikuu wafanye siasa vyuoni kwa taratibu zilizowekwa kwa sababu vyuo ni kitovu cha mabadiliko ya jamii ikiwa ni pamoja na kuwa chimbuko la viongozi mbalimbali

Wito huo umetolewa leo na Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu ambapo amekinzana na kauli ya Rais  Magufuli aliyoitoa siku chache alipotembelea Chuo cha Kilimo cha Sokoine kuwataka wanafunzi wasifanye siasa vyuoni.
Kiongozi huyo amesema "Kupiga marufuku siasa vyuoni ni kujenga taifa la vijana waoga, wasiokuwa na uwezo wa kuhoji.  Vijana msiache kuhoji mambo ya msingi kwa jamii zenu, hiyo ndiyo maana ya usomi" na kwamba maisha ya siasa wakiwa vyuoni ndiyo yaliwapa ujasiri wa kuingia kwenye ulingo wa siasa. 
Mbali na hayo Chama hicho kimeshauri kuwepo kwa mfumo mpya wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, kutokana na mfumo uliopo sasa kutokidhi mahitaji ya wanafunzi hali inayopelekea wengi wao kukosa mikopo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo