"Tumpe nafasi Magufuli atunyooshe" - Polepole

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM , Ndg Humphrey Polepole ametaka Rais Magufuli apewe muda kwanza wa kunyoosha na kurejesha misingi ya utaifa kabla hajagusa kwenye suala la mchakato wa Katiba Mpya

Polepole ametoa kauli wakati alipokuwa akifanya majibizano katika ukurasa wake wa twitter ambapo amesema kuwa yeye hakuwahi kusema Katiba inayopendekezwa ni nzuri hivyo rais anapaswa kupewa muda wa kuimarisha nchi na Ukatiba.
"Aliyesema Katiba Inayopendekezwa nzuri nani? Ilipatikana bila muafaka, maridhiano na uelewa wa pamoja. Tumpe nafasi Ndg. Magufuli atunyooshe, aturejeshee misingi ya Utaifa, hasa nidhamu ya sisi viongozi na umuhimu wa kuheshimu watu. Saizi tujenge nchi na kuimarisha UKATIBA", Polepole.
Oktoba, 20014 Bunge maalumu la Katiba nchini Tanzania lilipitisha rasimu ya katiba iliyopendekezwa ambapo kabla ya kupitishwa kwa rasimu hiyo, bunge hilo maalum lilikaa kama kamati kujadili mapendekezo katika Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na tume hiyo ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya uongozi wa Jaji Joseph Warioba.
Zoezi hilo la upigaji kura ambalo lilianza Septemba 29 mpaka Oktoba 2, siku matokeo yalipotangazwa, lilisusiwa na wabunge wengi wa upinzani, kwa madai kuwa baadhi ya vipengele vya awali vilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyopewa kazi ya kukusanya maoni kutoka kwa mwananchi, vilikuwa vimeondolewa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo