Rais Magufuli: Polisi Fanyeni Lolote

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka jeshi la polisi kufanya lolote lililopo ndani ya uwezo wao, ili kuhakikisha amani ya nchi haivunjwi na kubaki na utulivu

Kauli hiiyo imetolewa leo jijini Arusha alipokuwa akihutubia kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, na kusema kwamba anatambua kazi ya jeshi la polisi ingawa kuna watu ambao wana wabeza, hivyo wasiyumbishwe na watu hao, ila waendelee kuchapa kazi kwani yeye kama Amiri Jeshi Mkuu wao yuko pamoja nao.
Kuna watanzania wanaongea maneno ya kebehi kebehi kuhusu polisi, hawajui thamani ya polisi, ndugu zangu polisi tembeeni kifua mbele, na kwa bahati nzuri mimi ni shemeji yenu, mkwe wenu, msiwe na wasi wasi, maneno ya kashfa na kebehi yanayozungumzwa na wengine wala yasiwakatishe tamaa. Nilipopewa urais nikaapa kuhakikisha nchi inakuwa salama, na kuhakikisha nchi inakuwa salama, lazima jeshi la polisi liwe salama, endeleeni kuilinda amani ya nchi yetu, mtakayoyaamua yaamueni na mimi nitawasapoti, niliapa kuilinda amani ya nchi hii kwa nguvu zote na nitailinda”, amesema Rais Magufuli.
Sambamba na hilo Rais Magufuli amesema anatambua mazingira magumu waliyonayo askari polisi hususan wa vyeo vya chini, hivyo atahakikisha anatatua kero zao ikiwemo kuboresha makazi yao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo