Rais Magufuli amfuta kazi Mkurugenzi

Rais Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Mohamed Maja kuanzia jana kutokana na kushindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato na kuisababishia halmashauri hiyo upotevu mkubwa wa fedha za serikali

Hayo yamebainishwa na Katibu mkuu wa ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Tamisemi Mussa Iyombe wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma na kusema utenguzi huo umefanyika ili kutoa nafasi ya kufanyika uchunguzi juu ya tuhuma hizo.
Iyombe amesema tume iliyoundwa kufanya uchunguzi wa utendaji katika ofisi ya mkurugenzi huyo imebaini baadhi ya fedha zinapotea mikononi mwa watu na mkurugenzi huyo kushindwa kudhibiti.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Tamisemi Josephat Kandege, amewataka wenyeviti wa halmashauri kote nchini kuzingatia mafunzo waliyopewa na uongozi wa chuo cha serikali za mitaa hombolo ili wawe mabalozi bora katika maeneo yao


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo