Mwanamke aliyetelekezwa na Mchina avilaumu vyombo vya habari

Safina Mohamed
Sasa leo Jumanne Aprili 10, 2018 mama huyo aliyetambulika kwa majina ya Safina Mohamed ameibuka na kuvilaumu vyombo vya habari kwa kusambaza picha za mtoto wake kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo amekiri wazi kuwa ni kinyume na maadili.
Nia na malengo na madhumuni ya kunileta hapa ni kutafuta haki ya mtoto wangu, kama watoto wengine ambao wakiafrika waliotelekezwa kwa maana hiyo nasikitika sana kwa mitandao ya kijamaa kwa kutoa taarifa ambazo ni tofauti na zile zilizonileta hapa, na nasikitika kwa nini picha za mtoto wangu zinasambazwa? kwa hiyo naomba jamii isinichukulie mimi vibaya mimi nataka haki ya mtoto wangu,“amesema Bi. Safina mapema leo mbele ya Waandishi wa Habari kwenye ofisi za mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.
Bi. Safina amesema alipotezana na mumewe aliyemtaja kwa jina la Zhou Quin aliyeondoka nchini baada ya kibali chake cha kufanya kazi nchini kuisha mwaka 2016, na mpaka sasa hana mawasiliano naye.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo