Godbless Lema Amshangaa RC Gambo Kumuita Rafiki

Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema hajasita kuweka wazi hisia zake baada ya kutambulishwa na RC Gambo katika Ibada ya kusimikwa Mhashamu Isaack Amani kuwa Askofu Mkuu Jimbo la Katoliki la Arusha.

Lema kupitia ukurasa wake wa Twitter ameonekana kushangaa kitendo cha RC Gambo kumuita yeye rafiki.

Ameandika; “Katika Ibada ya kusimikwa Askofu, Rais aliongea neno la Mungu kuhusu Amani na Haki. Bila shaka demokrasia na haki vitashamiri tena. Askofu Amani yeye akasisitiza ushirikiano kisiasa bila kubaguana. Mrisho Gambo(RC) yeye akuogopa kuwa muongo madhabauni, eti aliniita Mimi rafiki yake."


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo