Prof. Assad ameyasema hay oleo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akikabidhi ya ukaguzi wa hesabu za serikali ya mwaka wa fedha ulioisha wa 2016/17 kwa Rais John Magufuli.
Miongoni mwa vyama vilivyotajwa ni pamoja na chama cha Demokrasia Makini, TLP na ADC.
“…Chama cha Demokrasia Makini, Alliance for Democratic Change na Tanzania Labour Part, vyama saba vilivyopata hati chafu, sheria inatutaka sisi tukague vyama vya siasa, iwe vinapata ruzuku havipati ruzuku ni jambo lingine kwa namna hiyo tumetoa muhtasari wa vyama vya siasa,” Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Assad.