Tazama Mahafali ya 3 ya Kidato cha 6 Lupalilo Sekondari Yalivyokuwa

 Wanafunzi wa kidato cha 6 ambao ndio wahitimu wakiingia Ukumbini

 Wanafunzi hao wakisoma Risala


 Mgeni rasmi akitoa hotuba yake
WANAFUNZI wa kidato cha sita katika shule ya sekondari Lupalilo wilayani Makete mkoani Njombe wameeleza furaha yao baada ya kusherehekea  mahafali yao ambayo ni ya tatu yaliyofanyika jana shuleni hapo

Wakizungumza nasi katika sherehe za mahafali hayo shuleni hapo,  wanafunzi hao wamesema hatua waliyoifikia kwa sasa ni hatua nzuri katika kuelekea kutimiza ndoto zao.

Aidha wameongeza kwa kuwaasa wanafunzi wengine walio katika ngazi ya chini kuwa ili kufikia hatua yoyote maishani jambo la msingi ni kuwa na jitihada na uvumilivu.

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo mwalimu Johnes Liombo amesema  mwaka 2016 walipokea wanafunzi 215 ambapo wengine walihama na wanaotarajia kuhitimu kidato cha sita ni zaidi ya wanafunzi 170, na kuongeza kuwa  lengo la kufanya mahafali hayo mapema ni kuhakikisha wanafunzi wanakuwa na muda wa kutosha wa kufanya maandalizi ya mitihani yao ya mwisho.

Katika mahafali hayo mgeni alikuwa ni kaimu  mkuu wa TAKUKURU wilaya ya makete  Bw, Topela Kashinde ambapo naye amesema serikali inafahamu fika changamoto zinazowakabili wanafunzi hao  na ipo katika uangalizi mkubwa.

Wanafunzi wa kidato  cha sita ndani ya mwezi wa tano mwaka huu wanatarajia kufanya mtihani wa taifa ambao ni mtihani wao wa mwisho


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo