Nondo afananishwa na Viongozi

Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amewataka watanzania kupiga kelele ili sheria ichukue mkondo wake hasa katika masuala ya watu kubambikiwa kesi

Mh. Heche ameamua kusema hayo baada ya Mwanafunzi Abdul Nondo kupotea jijini Dar es salaam kisha kupatikana huko Iringa  na habari tofauti zikiibuka kwamba alijiteka na kudaiwa kwamba alitoa taarifa za uongo.
Kutokana na taarifa hizo Mbunge wa Heche amesema kwamba "Kama viongozi  wanabambikiziwa kesi mchana kweupe sio ngumu kwao kumtengenezea huyu kijana kesi".
Ameongeza kuwa "Ni  wajibu wa Watanzania wote kupiga kelele sheria ifuatwe kwenye sakata hili".
Nondo, ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) aliripotiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha tangu siku ya Machi 8 , ambapo amepatikana akiwa ametupwa barabarani Mafinga mkoani Iringa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire, amesema Nondo amepatikana akiwa salama bila jeraha lolote wala kupigwa lakini wamefungua jalada hilo kwa ajili ya uchunguzi na mpaka sasa bado yupo kituoni hapo na iwapo atabainika alidanganya atashughulikiwa kama wahalifu wengine.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo