Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania Ajiuzulu

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga ametangaza kujiuzulu wadhifa wake kwa sababu binafsi.

Taarifa ya TEF iliyotolewa leo Machi 17, 2018 imesema: “Makunga amechukua hatua hiyo kwa kutumia uhuru wake binafsi kama mwanachama wa TEF.” Imesema kutokana na uamuzi huo, mkutano mkuu wa dharura wa TEF uliokutana leo umeridhia kujizulu kwake huku ikieleza TEF itakosa uongozi na busara za Makunga ambazo zilikuwa bado zinahitajika kwa ajili ya ujenzi wa tasnia hii ya kitaaluma. Kutokana na kujizulu, Makamu wake, Deodatus Balile atakaimu nafasi ya Makunga hadi taratibu za kujaza nafasi hiyo itakapokamilika.

Tazama hapo chini:-


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo